GET /api/v0.1/hansard/entries/1186837/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1186837,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186837/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ahsante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Ninaunga mkono Taarifa ya Sen. Madzayo kuhusiana na kufurushwa na ubomoaji wa makaazi katika maeneo ya Pindukiani Ward katika Kata ya Ganda, Kaunti ya Kilifi. Hili limekuwa donda sugu. Hata mimi siku ya Ijumaa wiki iliyopita, nilipigiwa simu ofisini mnamo saa kumi na nusu, nikaelezwa kwamba kuna mama mzee mjane, aliyekuwa anafuruswa kutoka kwa nyumba yake katika mtaa wa Ganjoni eneo Bunge la Mvita, Kaunti ya Mombasa. Nilipofika hapo, ikawa mambo ni kama hayo anayoyazungumzia Sen. Madzayo. Dalali alikuwa amekuja na amri ya kutoka mahakama ndogo. Wakati yule mama alikuwa na amri ya kutoka Mahakama Kuu. Dalali yule hakuweza kuheshimu amri ambayo imetolewa na Mahakama Kuu. Masuala kama haya yanatokea licha ya kuwa sheria sasa imepanuliwa ili kulinda wananchi wanaotaka kufurushwa hivi. Hii ni kwa sababu huwezi kupata uzaidizi wa polisi kwanza mpaka uweze kupeleka amri ile kwao. Polisi wao badala waje waulize mhusika kama ni ukweli kuna amri ya kufurusha dhidi yake, polisi wanakwenda mahakani kuchunguza amri. Wakiona kuwa kuna amri kama hiyo wanakuja moja kwa moja kumhamisha mtu yule. Suala hili lazima liaangaliwe kwa undani zaidi. Hata kama itabidi lile jopo la madalali yafaa kuitwa katika Kamati hii ili waeleze ni kwa sababu gani hawawezi kutekeleza amri zile kwa njia ambayo itampa nafasi yule mhusika aweze kufuatilia mambo yote ya kisheria ambayo yatamwezesha asifurushwe na mali kuharibiwa kiholela. Tumeona sehemu nyingi, nyumba zimevunjwa. Juzi hapa Nairobi katika maeneo ya Westlands, nyumba na mali ya thamana ya karibu million sabini imevunjwa na kuvurugwa wakati kuna watu ambao kupata makao ni shida. Katiba yetu inatoa haki ya mtu kuwa na makao ambayo ni salama na ya kufaa. Tukipambana na madalali kama hawa ambao wameenda huko Pindukiani, haki ile imekuwa ni kama hewa moto ama hot air. Ninaomba kamati hii itakapochunguza suala hili, iwaite wale wahusika madalali waje wajieleza ni kwa sababu gani hatua za kisheria haziwezi kuchukuliwa kwa yule amabye amehusika na masuala kama hayo. Mwisho, ninampongeza Sen. Korir kwa kuchaguliwa kama Naibu wa Mwenye Kiti wa Tume ya Bunge. Ninafikiri Imekuwa ni ndoto kwake lakini yametendeka. Sisi tutakuunga mkono katika kazi zako ili tuhakikishe kwamba unazitekeleza ipasavyo. Ningempa pole ndugu yangu Sen. Cherarkey. Nimeona katika baadhi ya mitandao, inasema kuwa alipigwa kabari hapa mjini Nairobi. Pole sana Mhe. Sen. Cherarkey."
}