GET /api/v0.1/hansard/entries/1186842/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1186842,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186842/?format=api",
    "text_counter": 189,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "Ni masikitiko kwamba mambo kama hayo yanazidi kuendelea. Watu masikini wanafurushwa kwenye ardhi zao kiholela. Kuna sheria ambazo zimewekwa. Tulipopitisha Katiba mpya, tulitengeneza National Land Comission (NLC) ambayo inafaa kuhakikisha na ithibitishe kwamba mambo kama hayo hayafai kutokea kwa sasa baada ya hiyo Tume kuwekwa. Tume hiyo ilikuwa inafaa iangalie historical injustices katika masuala ya ardhi na iangalie ya kwa kwamba hatimiliki zinatolewa kwa njia gani kuanzia chini kuja juu. Utakuta watu wanajitolea hatimiliki na wale ambao ni wamiliki halali wa hiyo ardhi wanakuja kufukuzwa kwenye ardhi zao kiholela bila thibitisho ya kusema kwamba huyu mwenye hii hatimiliki kweli ndiye mwenye hiyo ardhi ama ni yule mkaazi kwenye hiyo ardhi. Bi. Spika wa Muda, kuna haja kamili ya watu kujua njia na mbinu za kutafuta hatimiliki zao. Utakuta Wakenya wengi hawana uzoevu na kuelewa njia zinazofuatwa ili mtu apate hatimiliki kwa ardhi yake ambayo pengine ameipata kuanzia mababu na mababu. Ukosefu wa kuelewa mbinu za kupata hatimiliki umefanya watu wengi kudhulumiwa. Wengine ambao wana uzoefu, walio na mapesa na mabwenyenye wanaenda na kujitolea hatimiliki kwa ardhi ambazo sio zao kihalali. Kule Kaunti ya Lamu tuna mradi wa LAPSSET na miradi mingine mikubwa tunayotarajia Serikali kuyatekeleza. Hivi sasa kuna dhuluma kubwa ya watu kwamba ardhi zao zimechukuliwa. Wakulima na wengineo hawajapewa fidia yoyote. Vilevile vile, hawajapa chochote kusema kwamba wamelipwa ama watalipwa. Mpaka sasa hawajijui. Utakuta watu hawako katika mashamba yao karibu miaka minane au kumi iliyopita. Mashamba yao yaliyochukuliwa na Serikali kwa minajili ya kuanzisha miradi mbalimbali. Hatimiliki zimetolewa na makampuni na watu mpaka sasa wameachwa maskini hohehahe. Tunahimiza ile tume ya NLC iwajibike kuhakikisha yule mwananchi wa chini atapata haki yake. Tulipopitisha Katiba, hiyo Tume iliundwa na jukumu lake kubwa lilikuwa ni kushughulikia historical injustices . Hata hivyo, wao wanaonekana wamezembea kazini. Kamati ya Ardhi ihakikishe Tume hii iwajibike kuondosha dhuluma kana hizo. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}