GET /api/v0.1/hansard/entries/1186848/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1186848,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186848/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Ninakemea sana jambo hili la kuwafurusha watu wetu kwa nguvu kutoka ardhi wanamoishi. Waacheni tabia hii ya kuvunjia watu nyumba zao na kuzifanya familia zao na watoto kuteseka. Bwenyenye anakuja na title deed na kusema kuwa hiyo ardhi ni yake, amepewa. Sisi kama Maseneta katika Bunge hili tunatakikana tusimame pamoja zote tukemee hili jambo haswa la kuvurusha watu kutoka kwa ardhi yao. Mimi ninaunga mkono Taarifa jhii . Mimi ni mmoja wa Wanachama wa Kamati ya Ardhi. Wakati kulipotokea tatizo kama hili katika Kaunti ya Kwale, nilipeleka Kamati ya Ardhi katika shamba hilo kule Diani. Iwapo Taarifa hii itapelekwa katika Kamati ya Ardhi au nyingine kulingama na uamuzi wako, ikija katika Kamati yangu, tutahakikisha tumeenda kwa ardhi hiyo, tuione na tujue jinsi walivyopokonywa ardhi yao. Baada ya hapo, tutahakikisha kwamba wananchi wamepata haki yao."
}