GET /api/v0.1/hansard/entries/1186983/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1186983,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186983/?format=api",
    "text_counter": 330,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Spika wa Muda, kwa kunipa fursa ya kuchangia Hoja iliyoletwa na Sen. Mungatama, MGH, Seneta wa Kaunti ya Tana River. Masuala ambayo ameyazungumzia Sen. Mungatana, MGH ni mazito sana ikizingatiwa kwamba maji ni uhai na tumekuwa na maafa ya mara kwa mara katika eneo la Mto Tana, ikiwemo ukame ambao sasa unaendelea pakubwa. Vilevile, kuna mafuriko ambayo yanatokea mara kwa mara. Bw. Spika wa Muda, Mto Tana ni sehemu ambayo iko na nafasi kubwa ya kuinua uchumi wa Kaunti yake na hata nchi nzima kwa jumla. Hii ni kwa sababu mahali ambapo Mto Tana unaingia katika Bahari ya Hindi, ni eneo nzuri sana kwa kilimo cha samaki. Kwa Kiingereza wanaita aquaculture . Sasa maji yamezuiliwa na hayashuki kwenda chini Mto Tana. Inamaanisha kwamba nafasi ya kufanya aquaculture, utalii wa bahari na vilevile kwenye mto, imeambulia patupu. Mnamo miaka ya 1992 hadi 1997, kulikuwa na mwekezaji mmoja ambaye alikuwa anataka kufanya kilimo cha samaki kama vile kamba na wengine. Alikuwa na ekari 40,000 katika eneo hilo. Hata hivyo, kutokana na utepetevu wa Serikali na watu kutaka mlungula, ilibidi mradi huo uondolewe na kesi kuingia kortini. Hadi sasa, ninafikiri kesi zingine kuhusiana na swala hilo bado hazijaamuliwa. Kwa hivyo, ni eneo ambalo lina utajiri mkubwa ambao unaweza kutumika kuwatoa wakaazi wa Kaunti ya Tana River kutoka kwa janga la njaa na mafuriko. Haya ni maafa mawili ambayo yamewakabili miaka nenda, miaka rudi. Maji ambayo yametumika sasa kutokana na huu mradi wa Northern Tunnel Intake Project, kuenda Murang’a, Kiambu na maeneo mengine ya miji ya Nairobi, ni maji ambayo yangesaidia pakubwa maeneo ya Turkana hadi sehemu za Kitui na Garissa. Ni kwa sababu hiyo mto unapita hizi sehemu zote. Ilikuwa makosa watu wa sehemu hizi kutohusishwa wakati mradi huu ulipokuwa unapangwa na kutekelezwa."
}