GET /api/v0.1/hansard/entries/1186985/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1186985,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186985/?format=api",
"text_counter": 332,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Ninaunga mkono maoni ya Mhe. Ali Roba, kwamba kufanywe tena uchunguzi upya kuhusiana na mradi huu. Tuangalie hatari gani imeletwa kwa mazingira na wananchi wote, baada ya kuidhinishwa kwa mradi huu kuanzia sehemu ya juu kule ambako maji yanakwenda, mpaka sehemu ya chini ambayo ni mtoni, ambako maji yale yalikuwa yanafika kusaidia wananchi ambao wako katika sehemu zile. Bw. Spika wa Muda, mradi wa Galana-Kulalu ungesaidia pakubwa maswala haya. Mradi wa Bura ambao pia uko katika Kaunti ya Tana River, pia ungesaidia. Hii miradi yote imesalia kuwa kitendawili. Hadi sasa, miradi hii haijaleta latija ambayo iliyotakiwa. Kwa mfano, kilimo cha pamba katika eneo la Bura, hakijastawi mpaka sasa. Kilimo cha mahindi katika mradi wa Galana Kulalu vilevile mpaka sasa hakijastawi. Kwa hivyo hata wale wakulima ambao wako karibu na miradi hii, hawajafaidika na miradi ambayo imepangwa na kutekelezwa na Serikali. Lazima tuunge mkono Hoja hii wa Sen. Mungatana, MGH. Lazima tuzingatie kwamba kupoteza fursa za ukulima na njaa, ni maswala nyeti ambayo yataendelea kukabili kaunti hii kwa muda mrefu utakaokuja, bila kuwa na suluhisho lolote. Mbali na hilo, kuna mmomonyoko mkubwa wa udongo katika sehemu za Kipini, ambao utaharibu mazingira ya samaki kuzalia. Hii ni kwa sababu samaki wengi huingia ndani kwenye mito ambapo wanapata chakula kwa rahisina kuwacha watoto wao kuja kuzaa baadaye wakati mayai yameshaiva kutegua samaki. Hii itaathiri pakubwa mazingira katika sahemu zile. Tunapozungumzia mazingira, sio mazingira ya miti na binadamu peke yake. Hata viumbe vya baharini vitaweza kuathirika kwa sababu hii yote ni ile tunaita kwa kiingereza “eco system” ya eneo hili la Tana. Ikiathirika kwa upande mmoja, ni yote imeweza kuathirika, hususan, panapokosekana maji katika sehemu ile. Hii inamaanisha kwamba, ile sehemu yote imeweza kuathirika na hivyo basi wananchi, viumbe wa baharini, miti na wanyama wa nchi kavu watapata shida. Ili kupatikane mpango endelevu, haya maswala yamezungumziwa katika Hoja hii ya Sen. Mungatana lazima yaangaliwe kwa makini na kwa haraka. Mambo ya Serikali mara nyingi huchelewa hususan ikiwa lile lengo lilikuwa linatarajiwa limekwishapatikana. Kwa mfano, safari hii lengo ilikuwa ni kupeleka maji kaunti za Murang’a, Kiambu na Nairobi. Kwa hivyo kwa vile hawa wameshapata, basi wale wako kule chini Tana River, Kitui, Ijara wote waweze kusubiri hadi kutakapo kuja watu wengine. Hii haitaathiri peke yake kwa sababu ukiangalia sehemu zile zingine, kuna ukanda ambao kuna wale wanyama wanaitwa dolphins wanasafiri kutoka bahari kubwa na kupita katika ukanda ule sehemu fulani ya nchi. Wanapita pale kwa sababu kuna chakula fulani ambacho wanaweza kupata katika maeneo yale wakati wanapita. Hii ecosystem ni kubwa sana kiasi ambacho athari zake za muda mrefu zitakuwa kubwa na zitakuwa ni environmental disaster kwa eneo letu. Kwa hayo mengi, naunga kuunga mkono Mswada huu."
}