GET /api/v0.1/hansard/entries/1186999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1186999,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1186999/?format=api",
    "text_counter": 346,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika wa Muda. Nampa kongole Seneta wa Tana River, Sen. Mungatana, kwa kuleta Hoja hii. Kwanza, tangu tulipozaliwa, tunajua Tana River ni Kaunti ya Wapokomo. Ilibainika wazi Wapokomo ndio walioishi humo. Kwa sababu ya mchanganyiko, sasa tunakubali kwamba Tana River sasa imepanuka na vizazi vimekuwa vingi. Bw. Spika wa Muda, Mto Nile unaanzia Afrika Mashariki, kutoka Ziwa Victoria. Hata hivyo, hakuna nchi ambayo inapata faida ya huo mto isipokuwa Misri. Sisi sote hapa tumetembelea Misri na kuona wanafanya mambo mengi sana kutumia huu Mto Nile. Kwa nini hatuwezi kufanya hivi? Ni kwa sababu ya vigezo vya sheria za kitaifa. Ikiwa tunazingatia sheria zao na kuzijumuisha kuwa zetu, itakuwa muhimu pia tuheshimu vigezo hivyo. Ikiwa tunaheshimu Mto Nile, basi pia tuheshimu Mto Tana. Wakulima wanaoishi upande wa chini wa mto huo, wapewe nafasi ya kufanya kilimo chao ili wapate mazao ambayo wanaweza hata kuuza."
}