GET /api/v0.1/hansard/entries/1191119/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1191119,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1191119/?format=api",
"text_counter": 4108,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Kwanza, ningetaka kutoa rambirambi zangu za pole kwa dadangu kipenzi, Deputy Speaker Hon. Shollei. Poleni sana. Mjadala huu ambao umeletwa leo Bungeni uko na tamausho sana. Tuko na visa vingi sana vya saratani ndani ya Kaunti ya Mombasa. Utafiti uliotolewa hivi majuzi unaonyesha kwamba Mombasa inaongoza katika haya maswala ya saratani. Ningependa kuwaelezea kuwa vyakula tunavyokula vinasababisha saratani. Vyakula vilivyo ndani ya maduka yetu makuu vina athari nyingi. Unapoangalia kuku, ukimchinja nyumbani ukamweka mahali utampata kama amenyong’onyea, ilhali akiwa katika haya maduka makubwa, huwa amefura. Hii ni kwa sababu kuna zile kemikali ambazo kuku huwa wanadungwa katika hayo maduka makubwa. Siku hizi wakulima katika mashamba yetu wananyunyizia kemikali ambazo ni kali sana. Ndio maana tunaona akina mama wajawazito wanapata watoto ambao hawaeleweki, na wana mapungufu ya kimaumbile. Idara inayohusika lazima iangalie jambo hili, na watafute mbinu mwafaka ya kuzingatia sheria inayoweza kuthibiti mambo kama haya. Hii ni kwa sababu jambo hili limekuwa donda sugu ndani ya Taifa la Kenya sasa. Kama alivyosema dada yangu, Mhe. Shollei, sisi tulikuwa tunatoa pyrethrum hapa nyumbani. Kwa nini kampuni zetu na viwanda vyetu vya hapa nchini huwa vinafungwa kila siku? Inafaa kule Mombasa tupate viwanda vya korosho, sukari ama cha mnazi badala ya kutoa nazi kutoka India au China, ilhali hatujui kemikali gani zimewekwa ndani. Wasiwasi wangu mkubwa ni kwa sababu ya watu wangu wa Kaunti ya Mombasa. Akina mama wako na mitihani mikubwa. Ningependa kushauri hao wanaohusika kupitisha mambo haya kuwa waangalie sheria ambayo inaweza kuweka vizingiti na kudhibiti zile kemikali zinazotumiwa katika mashamba yetu kwanza. Yafaa Kenya Bureau of Standards (KEBS) iangalie kemikali zinazotumiwa katika vyakula vinavyoletwa kwenye maduka yetu makubwa. Sisi kama jamii tunaponunua bidhaa, tunapatwa na matatizo mengi sana. Namshukuru dada yangu kwa kuleta Hoja hii. Pia naunga mkono kuwa wale wanaofanya mambo haya wachukuliwe hatua."
}