GET /api/v0.1/hansard/entries/1191367/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1191367,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1191367/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Ripoti ambayo imeletwa Bungeni ya uteuzi wa wagombea wa ubunge wa EALA. Kwa hakika wote ambao wameteuliwa wanatajiriba. Ni vizuri tuchague watu ambao watakuwa na uwezo wa kusongesha mbele Bunge hili la Afrika Mashariki. Bw. Spika, tukiangalia katika zile taasisi za East Africa Cooperation, Mahakama ya East Africa imefanya maamuzi ambayo yamesaidia maswala ya haki za binadamu katika maeneo yetu kwa sehemu kubwa kuliko yale ambayo yamefanywa na Bunge hili. Hayo yote yametokana na maswala kwamba wale wanaoenda kutuwakilisha ni watu ambao wanaenda kutafuta kazi. Si watu wanaoenda kuangalia yale maswala ambayo yanaangaziwa na Bunge lile. Nimebahatika kusafiri kwenda Zanzibar na Pemba mwezi uliopita. Niliona kwamba kuna mambo mengi ambayo Bunge hili linaweza kuangazia ili kurahisisha biashara baina ya nchi saba za Afrika Mashariki. Kwa hivyo, wale ambao tutawachagua siku ya Alhamisi lazima wawe ni watu ambao wana maono ya kupeleka Bunge hili mbele, wala si kutafutia watu kazi. Hata kama mtu ndio mara yake ya kwanza kuchaguliwa, ikiwa ana maono ya kupeleka Bunge hili mbele, anafaa kupewa kazi hiyo. Kuna wengi ambao wamechaguliwa katika Bunge hili la Seneti mwaka huu, hawajakua Maseneta lakini tumeona zile kazi ambazo wamefanya zinaridhisha kwa sababu wamechaguliwa kusaidia nchi hii kwenda mbele. Asante."
}