GET /api/v0.1/hansard/entries/1191523/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1191523,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1191523/?format=api",
"text_counter": 366,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, nampa kongole Seneta wa Kaunti ya Kitui kwa kuweza kuleta Hoja hii. Imekuwa mtindo sasa katika sehemu fulani za nchi yetu ya Kenya ambako watu wanaleta mifugo, wanakuwa huru kuingia na kuweza kuyalisha hiyo mimea ya watu waliyotia bidi kuyapanda katika mashamba yao. Ni jambo la kusikitisha sana ikiwa mifugo hiyo inaharibu mali na mimea ya watu wa Kitui ambako kuna njaa. Watu wenyewe ni maskini lakini wamefanya bidi katika mashamba yao. Wamepanda halafu watu wengine wanakuja na ng’ombe, mbuzi na ngamia na kulisha katika mashamba yao ambayo siyo ardhi yao. Bw. Spika wa Muda, ni jambo la kusikitishwa. Haya yote yanafanyika bila polisi wa maeneo hayo kuchukua hatua yoyote. Wanataarifiwa kwamba, kuna watu fulani kutoka maeneo fulani ambao wamekuja na mifugo, wameingia nayo mashambani na kulisha mimea na kuharibu mali ya watu wengine bila wao kuchukua hatua yote. Hivi juzi, wiki hii hatujaimaliza, katika Kilifi Kaunti, katika eneo Bunge la Magharini, kijiji cha Kamale, kuna mashamba ya wananchi kule. Mashamba ya Wagiriama wamepanda mimea yao. Hao ni Mijikenda. Ni watu ambao wanategemea mimea yao katika mashamba yao kuishi. Leo, wamepanda mahindi yao hadi imekomaa. Imetokea ya kwamba watu wametokea sehemu zisizoeleweka wakiwa na mifugo yao. Wameingia ndani ya mashamba. Pia, wakitumia nguvu wakaingia ndani ya mto ambao watu wanateka maji ya kunywa. Ni watu ambao---"
}