GET /api/v0.1/hansard/entries/1191533/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1191533,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1191533/?format=api",
"text_counter": 376,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Inabidi binadamu wanakunywa maji pamoja na wanyama. Ngamia na ng’ombe wanakunywa hapo. Halafu wanawaingiza ndani ya mashamba ya Wagiriama wanakula mimea yao. Hii italeta vita ambavyo Serikali itashindwa kukomesha. Hatutakubali hata kidogo kuona watu wetu wanafanya bidii kulima na kupanda mahindi na vyakula vingine, halafu watu wengine wanakuja na ngamia au ng’ombe kuliwalisha mimea ambayo hawakufanyia bidii. Inatatikana Serikali ichukue hatua. Tuko na Seneta mchapakazi, Mhe. (Prof.) Kindiki, ambaye amechaguliwa juzi kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Tunamwomba aanze kazi yake ili asilaumiwe. Kenya hii sasa tunaona watu wengine wanadharau wenzao. Sisi kama watu wa Kaunti ya Kilifi, hatutakubali hata kidogo kuona mali yetu ikiharibiwa na watu wanaoleta mifugo katika mashamba yetu. Ni aibu sana kuona mtu anatoka kule anatoka na kuleta mifugo kwako. Akiulizwa, wanaua hawa watu au wanapigana nao. Hii ni tabia mbaya. Tunauliza hii Serikali sababu ina uwezo na iko makini, ichukue hatua kuona madhara kama hayo ambayo yanaweza kuleta vita vikuu nchini yamalizwe. Bw. Spika wa Muda, tumengojea Serikali iingilie kati lakini tumeshindwa na sasa tumechoka. We are tired! Tunaona watu wengine wakitumia mali yetu baada ya sisi kutumia nguvu kwa mashamba halafu wao waje kufaidika na mahali ambapo hawafai kufaidika."
}