GET /api/v0.1/hansard/entries/1192046/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1192046,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192046/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Taarifa ambayo imetolewa na Sen. Crystal Asige. Ninaunga mkono kauli iliyotolewa na Kiongozi wa Walio Wengi katika Seneti kwa sababu sheria nyingi zinatungwa na zile zinafaa kutungwa ndipo ziweze kutumika. Wahandisi wengi wanaopitisha ile michoro inayotumika katika ujenzi wa mijengo mingi katika kaunti, hawatilii maanani kwamba wanafaa kuzingatia sheria ili wale watu ambao wanaoishi na ulemavu wa wanaweza kuingia katika mijengo hiyo. Ninasema hivyo kwa sababu ukienda leo kuna michoro ya nyumba ambayo ilipitishwa na wahandisi lakini watu wanaoishi na ulemavu hawawezi kuingia ndani. Tunapoendelea kutunga sheria ambazo hazitiliwi maanani, hakuna kitu tutabadilisha katika nchi hii. Tunapotunga sheria na zile zilizoko za kusema kuwa majumba yajengwe yakiwa na nafasi nzuri ya usafiri kwa watu walio na ulemavu zizingatiwe vilivyo. Lazima Seneti ambayo ndio inaangalia maslahi ya kaunti tuhakikishe kuwa sheria hizo zinatumika vilivyo."
}