GET /api/v0.1/hansard/entries/1192056/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1192056,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192056/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "watoto walemavu. Mimi nimmoja wao kwa kuwa tuko na mmoja ambaye pia hali yake ni hali ya ulemavu na ya kusikitisha. Pia ingekuwa vyema kufikiria kuongeza idadi ya walimu wanaoweza kufundisha watoto walemavu. Ingekuwa muhimu kuhakikisha usalama wao hatari inapotokea. Wakati mwingine watoto hawawezi kutembea. kunaweza kuwa na hatari kama ya moto, mafuriko au nyumba kuporomoka. Itabidi wawe na haraka ya uzaidizi kuona kwamba madhara kama hayo hayatawapata watoto walemavu katika nchi hii. Mwisho, ninatoa kongole kubwa sana kwa rafiki yangu mmoja kule Mombasa - Bw. Hasu - ambaye ndiye mwenye ile kampuni ya Mombasa Cement. Ni kampuni ya kutengeneza simiti iliyoko katika kaunti yangu ya Kilifi. Sijaona binadamu kama huyo. Kenya nzima, ni yeye amejitokeza kwa nguvu zake zote kusaidia watoto walemavu. Ana shule kubwa inayoitwa Sahajanand Special School iliyoko Mtwapa,. Shule hiyo ina watoto walemavu zaidi ya 1,000. Kuna wale waioweza kuongea, kutemebea, kusikia na kuona. Ako na watoto walio na ulemavu wa aina mbalimbali. Anawachunga hao watoto wasiopungua 1,000 kwa hali na mali. Anagharamia elimu yao ikiwemo kulipa mishahara ya walimu. Wasioona kama dadangu, Sen. Crystal Asige, wanafunzwa na vifaa spesheli. Wasiosikia pia wanafunzwa kivyao. Wasio na uwezo wa kutembea lakini wanaona na kusikia, wanapewa mafunzo pia kwa shule hiyo."
}