GET /api/v0.1/hansard/entries/1192062/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1192062,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192062/?format=api",
"text_counter": 79,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ninakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia Taarifa hii ya Sen. Crystal Asige. Watoto na watu wazima wanaoishi na ulemavu wanakumbwa na shida nyingi haswa wanaposafiri. Usafiri ni mgumu kwao kwa sababu wanatembea na kusafiri kwa njia ngumu sana. Wanaosukumwa kwa wheelbarrows na wheelchairs wanapata matatizo mengi sana wanaposafiri. Ni lazima amri itolewe ili waweze kulindwa. Watoto aina hii wanapoenda shuleni, pia wanapata matatizo mengi upande wa mawasiliano haswa wale visiwi. Walimu nao hawawezi kuwafunza kwa Lugha ya Ishara ambayo wangefahamu. Wanapitia shida hata upande wa vyakula. Wengi wao wamezaliwa katika familia zisizojiweza. Unapata mama hawezi kuondoka nyumbani kwa sababu akiondoka, yule mtoto atabaki bila mtu na anaweza kubakwa. Mama hawezi kutoka kwenda kumtafutia yule mtoto chakula. Kwa hivyo, mama na watoto wanakosa chakula. Ninaomba Serikali iangalie zaidi familia zenye watoto walemav. Serikali iangalie mapato yao na ikiwezekana, hizi familia zisaidiwe ili kujikimu kimaisha na hata kusomesha hawa watoto."
}