GET /api/v0.1/hansard/entries/1192067/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1192067,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192067/?format=api",
    "text_counter": 84,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyowasilishwa na Sen. Crystal Asige. Naunga mkono Taarifa hii ya Sen. Crystal Asige kwa sababu mambo yanayoangaziwa katika Taarifa hii ni ya kimsingi. Nilibahatika kuwa mwanachama wa Rotary Club of Mombasa. Kila baada ya wiki mbili, huwa tunakwenda kuwalisha watoto walemavu katika Shule ya Port Reitz. Ukiona wale watoto wanavyoishi, utagundua kwamba ipo haja ya kuwasaidia ili waishi angalau maisha mazuri kidogo. Wakati tunapokwenda kuwatembelea wanafunzi katika Shule ya Port Reitz ambayo ni ya watoto walemavu, huwa tunapata kuwa walimu hawatoshi ukilinganisha na idadi ya wanafunzi. Mbali na kuwapelekea chakula, sisi pia huwalisha watoto wale ili kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata chakula cha kutosha. Madarasa yaliyojengwa ni ya kawaida ambapo mtoto mlemavu hawezi kuyafikia. Vile vile mahali pa kwenda kujisaidia hapajatengenezwa vizuri ukizingatia kuwa watoto hao ni walemavu. Kwa hivyo, mambo yanayopaswa kufanywa yatasaidia pakubwa kuhakisha kwamba wanafunzi wenye ulemavu wanakuwa na nafasi sawa kama wanafunzi wengine. Ningependa kusema kuwa Mhe. Hasu wa Mombasa Cement ametoa mchango mkubwa kwa watoto walemavu. Amejenga shule ambayo ndio kubwa katika Bara la Afrika kusaidia watoto walemavu. Shule hiyo ina karibu watoto 1,500 ambao wanakula na kulala pale. Wengine wana ugongwa unajulikana kama microcephalus. Ukiangalia kichwa ni kidogo kuliko kichwa cha mtoto wa kawaida. Hao ni tofauti na wale ambao wana vichwa vikubwa ambao wanajulikana kama hydrocephalus kwa Kiingereza. Sijui kwa Kiswahili wanaitwa vipi. Bw. Spika, utatusaidia hapo. Wale wenye vichwa vidogo wanajulikana kama microcephalus. Ukiwaona, utajua kwamba Mwenyezi Mungu huumba amtakaye kwa njia ambayo anaona ni sawa. Watoto hao wote wako katika shule ya Mhe. Hasu na pale wanapata kila kitu. Nafikiri kuwa hata Serikali haijafikiria kuwasaidia watoto kama hao. Watoto kama hao hawako katika sehemu za Pwani pekee kwa sababu wanapatikana kote nchini Kenya. Ikiwa kuna wazazi ambao wana watoto walemavu kama hao, ni bora wawapeleke kule ili waweze kusomeshwa."
}