GET /api/v0.1/hansard/entries/1192132/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1192132,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192132/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, unilinde kwa sababu haya mambo ninayozungumzia hapa ni mambo ambayo ni nyeti na yanaathiri sana watu wa Kaunti ya Mombasa. Ni wazi kwamba tunao utafiti ambao umefanyika na hata ikitakikana, ninaweza kuwasilisha stakabadhi hapa jumanne ya kuonyesha athari za Miraa na Muguka. Hatusemi kwamba ni biashara kwa hivyo watu wafanye. Kama ni biashara anzeni kununua nyinyi wenyewe kwanza Kaunti za Meru, Embu na Tharaka Nithi. Uzianeni kwanza kule mpaka iwaenee ndipo mtuletee sisi Kaunti ya Mombasa. Haiwezekani kwamba mmea kama huu ambao unaathiri vijana wetu uruhusiwe kuuzwa kiholela kama unavyouzwa sasa. Ninaunga mkono Kaunti yetu ya Mombasa iongeze kodi ya mimea hii miwili ili tuweze kulinda vizazi vijavyo vya watu wa Kaunti ya Mombasa na Kaunti zingine jirani kama vile Lamu. Hata katika Kaunti ya Lamu, mimea hii miwili imeathiri sana jamii. Hatuwezi kunyamaza hapa na kusema kwamba kwa kuwa watu wananapata chakula na wanalipa school fees --- Kwetu sisi ni kama biashara haramu."
}