GET /api/v0.1/hansard/entries/1192740/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1192740,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192740/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "aliendeleza suala hili kupitia Mswada. Namuhakikishia KJ kuwa tutalipatia kipao mbele litakapokuja kwenye Kamati ya NG-CDF. Hili ni jambo la muhimu na litaweza kusuluhisha matatizo na kubadilisha tetesi tulizonazo katika maeneo bunge yetu. Ninajua kijana anayeitwa Hassan Noor, ambaye alinialika kwake nyumbani. Nilipofika alinionyesha vile anaweza kugeuza moshi na kuufanya mwangaza wa taa—moshi uleule wa kawaida ambao unapatikana takriban katika kila jumba. Moshi unapatikana katika sehemu zetu nyingi, labda isipokuwa kwa Mhe. KJ, ambaye kwake ni mjini. Pengine hapa hakuna moshi kwa kuwa watu hutumia stima na gesi. Moshi unapatikana katika sehemu ambako Wabunge wengi wanakotoka. Mbali na kuona na kufurahia ujuzi huo, na kumpa chochote akanunue sukari—kama nilikuwa nacho siku hiyo—hakuna jambo jingine zaidi ningeweza kumsaidia kama Mbunge wa eneo lake. Ninajua taaluma kama hizi ziko kila mahali. Tukiangalia katika maeneo ya Pwani, kuna taaluma ya kushona kofia ghali zinazouzwa kwa takribani Ksh20,000 hadi Ksh25,000. Mara nyingi kofia hizo hushonwa na akina mama lakini saa hii imekuwa vigumu kwa sababu ya ukosefu wa usaidizi kutoka kwa Serikali."
}