GET /api/v0.1/hansard/entries/1192743/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1192743,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192743/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Nilipoanza kuzungumza, Mhe. Naibu Spika alikuwa kwenye kiti. Sasa Mhe. Spika wa Muda ndiye aliye kwenye kitini. Nataraji nimehifadhiwa muda wangu kwa kuongezewa dakika sita zaidi kwa sababu ya ule wakati ambao singeweza kuzungumza. Mhe. Spika wa Muda, tunazo taaluma katika sehemu mbalimbali humu nchini—kama vile katika maeneo ya Pwani, na haswa katika eneo Bunge langu la Matuga. Walio na ujuzi wa kushona kofia kama ile Mheshimiwa amevaa pale mbele wako huko. Kofia hiyo huwa inagharimu Ksh20,000 iwapo bei ni rahisi zaidi. Ni kwa sababu sio rahisi kutengeneza kofia ile. Kwa sababu ya ukosefu wa mfumo wa Serikali wa kuhakikisha taaluma kama ile inazalisha kwa wingi, saa hii tuna kofia kama zile ambazo zinatoka Uchina. Unapoziangalia, huwezi kuona tofauti baina yake na kofia ambayo imeshonwa na Mkenya. Ni kwa vile Wachina wamesimamiwa na serikali na mashirika yao, na kwa hivyo kuleta kofia hizo kwa bei rahisi ya Ksh5,000 hadi Ksh6,000."
}