GET /api/v0.1/hansard/entries/1192744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1192744,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192744/?format=api",
    "text_counter": 92,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "Hii inamaanisha kwamba iwapo Mkenya aliye na taaluma angekuwa amesaidiwa angeweza kuzalisha na kuuza katika nchi mbalimbali. Hii ingeleta fedha kwake na hata kwa nchi nzima kwa sababu angeweza kuuza bidhaa zake katika nchi za kigeni. Tumeacha taaluma kama hizi zitumiwe na Wachina. Alafu wanaturegeshea bidhaa hiyo kwa bei nafuu. Wanabuni kazi kule kwao ilhali watu wetu wanakosa kazi. Kwa hivyo, Hoja hii ni muhimu ili tuweze kubadilisha sheria ndiyo tupate usimamizi bora utakao wawezesha vijana wetu kutumia taaluma zao. Kama walivyosema walionitangulia, mara nyingi watu wanakuja kwa Wabunge. Inabidi wafanye hivyo kwa sababu hazina tunayozungumzia – kama vile Uwezo Fund, WomenEnterprise Fund na Youth Enterprise Development Fund – ziko maofisini na watu wengi kule vijijini hawazifahamu. Hawana njia ya kuweza kujua lolote kuhusu hazina hizi. Lakini wakati wote, hazina inapomhusu mbunge, kwa sababu yeye mwenyewe hutembea karibu kila mahali, basi moja kwa moja, huwa inanufaisha watu wengi na inawasaidia wale ambao wanahusika zaidi. Kwa sababu muda umekuwa adimu, ningependa kutoa kongole na kusema nauunga mkono Hoja hii ili iweze kuwa sheria ndiyo inufaishe nchi nzima kwa jumla. Asante, Mhe. Spika wa Muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}