GET /api/v0.1/hansard/entries/1192756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1192756,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192756/?format=api",
"text_counter": 104,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuunga mkono Hoja iliyoletwa na ndugu yangu, Mhe. Kiarie. Hoja hii inapendekeza kuangaziwa kwa maslahi ya wasanii wetu, na haswa suala la kuwapatia fedha za kuwawezesha kukuza vipaji vyao. Hoja hii imekuja wakati unaofaa kwa maana tuko na shida kubwa ya ukosefu wa kazi humu nchini. Vijana wengi humu nchini wamesoma lakini hawana ajira. Wengi wao wako na talanta tofauti tofauti ambazo kama zingeweza kufadhiliwa, tungekuwa tumepunguza ukosefu wa kazi. Inafaa pia ijulikane kwamba Mhe. John Kiarie, ambaye ameleta Hoja hii, alikuwa mbunifu sana katika mambo ya usanii alipokuwa chuo Kikuu. Alikuwa na kikundi kilichoitwa Redykyulass. Tulipokuwa naye katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, tulimuenzi sana. Kupitia juhudi zake, leo hii ninaweza kusema kwamba msanii anapofikia kiwango cha kuweza kushiriki kwenye utunzi wa sheria na"
}