GET /api/v0.1/hansard/entries/1192758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1192758,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192758/?format=api",
"text_counter": 106,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": null,
"content": ", anawakumbuka wenzake walioko nyuma. Bila shaka, Bunge la Taifa limepata mtu muhimu anayezingatia maslahi ya wasanii, na haswa vijana wetu ambao wako na vipawa. Mwenyezi Mungu ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza. Yeye ndiye kielelezo kikuu cha ubunifu unaoendelea mpaka hivi leo. Mwenyezi Mungu aliweza kuumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, akiwemo binadamu. Ameumba vitu vyote tunavyoviona na vile tusivyoviona. Kila alichofanya Mwenyezi Mungu kilikuwa sanaa ya hali ya juu sana. Ninaamini kwamba usanii uko na baraka fulani kutoka kwa Mwenyezi Mungu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}