GET /api/v0.1/hansard/entries/1192759/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1192759,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192759/?format=api",
    "text_counter": 107,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": "Sisi, kama Wajumbe, tuko na jukumu kubwa la kuwashika mikono vijana wetu walio na ubunifu aina mbali mbali. Mara nyingi tunapozungumzia usanii, watu wengi hufikiri tunazungumzia waimbaji peke yake. Cha muhimu ni watu wajue kuwa tuko pia na sanaa tofauti tofauti kama vile uchoraji. Kuna vijana ambao wako na tajriba kubwa katika uchoraji. Sanaa kama hiyo haijapewa kipaumbele nchini Kenya. Katika nchi za nje, na haswa nchi za magharibi, wasanii wa uchoroji wamebobea sana. Kiwango cha asilimia 2 kilichopendekezwa kwenye Hoja hii inayojaribu kuwatafutia vijana pesa za kuwasaidia kukuza vipaji vyao vya ubunifu ni kidogo sana. Iwapo Hazina ya NG-CDF itatenga asilimia 2, inafaa vijana watengewe asilimia kubwa kutoka kwa hazina ya Hustler Fund ili waweze kujiajiri. Mhe. Spika wa Muda, katika Eneo Bunge langu la Wundanyi, kuna vikundi vya vijana wanaojiita Taita Upcoming Talent na Vigogo Media, ambao wamebobea sana. Niko na vijana wa mzuki pia, na mmoja wao anajiita Babas Millionaire . Hao ni wasanii ambao tukiwashika mikono kiukweli, watapiga hatua kimaisha. Wataweza kuwaajiri vijana wenzao na hali ya usanii nchini Kenya italeta ajira kubwa itakayotuwezesha kupiga hatua ya kimaisha. Usanii utakuwa na uwezo wa kuleta ajira kubwa ambayo itatuwezesha kupigana na janga la ukosefu wa kazi. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii nikiwaomba Wabunge wenzangu tuipitishe haraka ili iweze kuwa sheria."
}