GET /api/v0.1/hansard/entries/1192794/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1192794,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192794/?format=api",
    "text_counter": 142,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Makueni Kaunti, WDM",
    "speaker_title": "Mhe. Rose Mumo",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa nafasi hii uliyonipatia nichangie Hoja hii ambayo ni muhimu sana kwa Wakenya. Ninamshukuru Mhe. Kiarie kwa kuileta Hoja hii ambayo itasaidia sana. Tumeona wasanii wengi katika nafasi za uimbaji, uigizaji na wale ambao wako na talanta za kutengeneza vitu, lakini Serikali haijachukua hatua kubwa ya kuangalia ni vipi ingeboresha usanii huu. Tangu tukiwa wadogo, tulimwona Mzee Ojwang’, ambaye amelala, Mama Kayai, na wengineo katika kipindi cha Vioja Mahakamani wakitufurahisha kwenye televisheni. Lakini ukifuatilia maisha yao ya baadaye, hayapendezi. Ilichukua nchi za ng’ambo kujua tuko na msanii mzuri kwa jina la Lupita Nyong’o na akasifiwa dunia nzima. Hii ni kusema kwamba Kenya tuko na wasanii na talanta mbali mbali. Serikali ingechukua nafasi kuwasaidia hawa wasanii ili waweze kubobea. Tukiwa nyumbani, tunaangalia filamu za Nigeria kwa sababu Serikali yao iliwapatia nafasi. Katika sekta ya muziki, Tanzania na Congo wamebobea. Kenya iko na wasanii wanaoweza kuimba. Wengine ni wa mchezo wa kuigiza. Lakini kwa sababu Serikali haijachukua nafasi ya kuwasaidia kuboresha kile ambacho wanajua, unakuta ya kwamba wanafifia halafu wanaondoka jukwaa. Wamebaki tu kutangazwa katika televisheni na magazeti na inaishia hapo. Kwa hivyo, namshukuru sana Mhe. Kiarie kwa Hoja hii ili tuhimize Serikali itenge pesa za kuwasaidia wasanii. Ukitaka kuelewa kwamba Kenya kuna wasanii wa kipekee, ukienda pale Gikomba utapata kuna mambo wanafanya kwa ustadi sana lakini yanabaki pale pale. Hawana namna ya kuyaboresha yaweze kuwa na manufaa zaidi na kufikia nchi za nje. Ninakumbuka wamama waliokuwa wanashona viondo zile za zamani. Kwa sababu hakukua na pesa za kuboresha kazi hiyo, usanii huo ulichukuliwa na watu wa Japan na sasa watu wananua viondo kutoka nchi hiyo. Kuna wale ambao wamesomea talanta hizi na kuna wale ambao wamezaliwa na talanta za kipekee. Serikali ingechukua hatua kuona jinsi inavyoweza kuwasaidia kuboresha talanta zao. Shule pia zinafaa kuchukua hatua makusudi ya kutambua mwanafunzi ambaye ako na talanta ya kipekee ambayo inaweza kukuzwa na iwe na manufaa kwa Kenya. Ninaamini kuwa Hoja hii itatekelezwa na pesa kutengwa ili wasanii watambulike. Pia, itasaidia kwa nafasi za kazi kwa maana sio wote wataenda kwenye maofisi. Wengine watajiandika wenyewe kwa sababu ya talanta mbalimbali ambazo Mwenyezi Mungu amewapatia. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}