GET /api/v0.1/hansard/entries/1192814/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1192814,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1192814/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Mjadala ulioletwa na ndugu yangu, Mhe. Kiarie, unahusu wanasanaa wengi ambao wamehangaika sana. Katika majumba yetu sisi, tunapenda sana kusifu na kutukuza wanasanaa kutoka mataifa ya nje ilhali wanasanaa wetu wanazorota kwa umasikini licha ya kuwa na muziki na uigizaji mzuri na mtamu sana. Mimi Mama Zamzam Chimba Mohamend, na Mama Kaunti, nina vijana wangu wa Mombasa wanaoigiza, imba na kufanya sanaa tofauti tofauti. Ningependa kumpongeza ndugu yangu kipenzi, Mhe. Kiarie, kwa kuleta Hoja hii. Najua kuna wakati ulikuwa mwanasanaa. Naunga mkono ili wanasanaa wapewe pesa ili waweze kuinuliwa kisanaa na kujiendeleza. Pole sana Mhe. wa Kwale. Zamu ikiwa yangu, ni yangu tu. Au vipi? Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii."
}