GET /api/v0.1/hansard/entries/1193008/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193008,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193008/?format=api",
    "text_counter": 134,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": ". Naibu Spika, asante kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Hoja ya kumteua Eng. Koome kama Inspekta Mkuu wa Polisi. Naunga mkono hoja hii kwa sababu kulingana na Ripoti ambayo imeletwa hapa Bungeni na Kamati Maalum, Eng. Koome ana tajiriba ya kuchaguliwa kama mkuu wa kikosi cha polisi nchini Kenya. Ujuzi wake na miaka yake mingi aliyofanyaka kazi ya polisi inampa uzoefu wa kufanya kazi hii bila matatizo yoyote. Kikosi cha Polisi kina changamoto nyingi. Kwa mfano, kule kwetu Mombasa kuna changamoto ya matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana. Mihadharati hii inauzwa na watu wakubwa ambao wana uwezo wa kuhonga polisi kiasi ambacho dawa zinauzwa kiholela. Mikakati mingi ambayo sisi kama viongozi tumeweka kupambana na dawa hizi imeambulia patupu. Hii ni kwa sababu polisi wakiwakamata watu hawa mara nyingi huwaachilia kwa sababu ambazo si za kimsingi. Tunatarajia kwamba afisa huyu mpya atakayeteuliwa ataweza kupambana na hili janga la dawa za kulevya Mombasa na Pwani nzima kwa jumla. Vile vile, kulikuwa na vilio vya mauwaji ya kiholela na kutoweshwa kwa vijana hususan wale wanawosemakana wana itikadi kali. Hili ni jambo ambalo tumezungumzia mara nyingi. Ninafikiri kulingana na maelezo aliyotoa katika mahojiano yake juzi na jana, ana uwezo wa kulitataua tatizo hili ambalo ni kubwa. Vile vile, kuna tatizo la ufisadi katika ngazi za polisi. Ufisadi huu umekithiri sana katika vituo vya polisi ambapo badala ya kuhudumia wananchi vimefanywa ni vituo vya kukusanya hongo kutoka kwa wananchi ambao hawana hatia."
}