GET /api/v0.1/hansard/entries/1193010/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193010,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193010/?format=api",
    "text_counter": 136,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": ". Naibu Spika, ukishikwa na polisi kwa mfano Mombasa, hakuna njia ambayo unaweza kutoka bila kuwacha mapeni, kiwango cha chini kabisa kikiwa Kshs2,000. Swala la ufisadi lazima apambane nalo kwa sababu kikosi cha polisi kimezongwa na shutuma za ufisadi. Mwisho ni swala la usalama. Mitaa mingi katika Mombasa kwa mfano sehemu za Likoni na Kisauni, usalama umeharibika. Ikifika saa moja jioni kila mtu anakimbilia nyumbani kwake. Hii imetokana na upungufu wa maafisa wanofanya doria za jioni. Vile vile, kuna kutowajibika kwa vikosi vya polisi kwa maswala kama haya. Tunataraji kwamba atakapoteuliwa ataweza kupambana na hizi changamoto na nyingi nyingine ambazo zinawakumba wananchi wa Kenya. Jana kulikuwa na ripoti hapa Nairobi kwamba kunasehemu ambazo ikifika jioni saa moja huwezi kupita kama mwananchi ikiwa huna silaha. Tunatariji afisa huyo mkuu wa polisi ataweza kutatuwa changamoto hizi iliwakenya waweze kuishi kwa amani na usalama. Vile vile, ili wawekezaji waweze kuja hapa kufanya biashara na wananchi wetu waweze kupata ajira na biashara kwa wale ambao wanafanya."
}