GET /api/v0.1/hansard/entries/1193026/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193026,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193026/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa ninaunga mkono ripoti ya kuidhinishwa kwa atakayekuwa Mkuu wa Polisi, Bw. Koome. Ninaunga mkono kwa sababu yeye ni mtu aliye na uzoefu wa kazi hiyo. Nimemsikiza rafiki yangu, Sen. Wambua, akizungumza juu ya Bw. Koome. Ninakumbuka pia aliyekuwa Mkuu wa Polisi, Bw. Mutyambai, alipokuwa akiteuliwa, nilimsikia Sen. Wambua akituambia vile ako na uzoefu. Ni vizuri na alifanya kazi nzuri. Bw. Koome amekuwa na uzoefu zaidi na nina uhakika atafanya kazi nzuri na ndiposa ninaunga mkono. Bw. Naibu wa Spika, Bw. Koome anapaswa ashughulikie shida zilizoko katika sehemu zetu za Kenya. Ukitembea sehemu zetu za Kaunti ya Laikipia, unapata wafugaji haramu. Wamekuwa wakivamia mashamba na kulisha mimea kiholela. Si vizuri. Hivyo basi, Bw. Koome yuko na kazi ambayo anapaswa kutekeleza kwa haraka, baada ya kuithinishwa kuchukua hatamu za uongozi. Ningependa kushukuru Serikali ya Kenya Kwanza kwa sababu wamesema dhahiri shahiri kwamba Tume ya Huduma kwa Polisi itakuwa inapata pesa zake moja kwa moja. Kwa hivyo, Bw. Koome hatakuwa na sababu ya kutowajibika kwa sababu hatahitaji kwenda Harambee House kutauta hela hizo. Hivyo basi, sisi tunasisitiza kwamba akipitishwa, alivalie njuga swala hili la usalama. Wasifu wake unaonyesha ya kuwa amepanda ngazi katika Idara ya Polisi. Ameonyesha umahiri wake pia. Hivyo basi, mimi sina shaka ninapomngoja huko kwetu katika Kaunti ya Laikipia. Ukitembea sehemu kama Wangwachi na Ol moran, unapata vile wakazi wanakumbwa na ukosefu wa usalama. Na vile vile, kwa sababu atapewa hela moja kwa moja katika Idara ya Polisi, aangalie maafisa wanaoishi katika hali ya uchochole. Nimetembelea vituo vingi vya polisi na hivi karibuni nilikuwa mahali ambapo panaitwa Wangwachi. Ukiingia hizo nyumba za maafisa wa polisi, hata hazifai kuitwa nyumba. Maafisa wetu wanaishi katika hema. Hema yenyewe iko na maafisa wanne wanaoishi ndani, na ni wanaume. Nikawauliza iwapo wameoa na wakasema kuwa wameoa. Bw. Naibu wa Spika, sipaswi kukuambia vile nilivyoulizwa swali lililofuatia, kwa sababu ni aibu katika karne hii. Halafu baada ya haya yote, sisi tunawashtumu maafisa hao, ati wamezembea katika kazi yao. Yule afisa anaishi katika hali ya uchochole, umempatia bunduki na kumuambia afuate wakora. Atatafuata wakora ama ataenda kushughulikia tumbo yake? Kwa hivyo, Bw. Koome akichukua hatamu za uongozi, pamoja na kufuatilia maswala ya usalama wa Kitaifa, aangalie pia maisha ya uchochole ya askari."
}