GET /api/v0.1/hansard/entries/1193031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193031,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193031/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii kuunga mkono Hoja ya kumpitisha Eng. Koome kuwa inspekta mkuu wa polisi katika Jamhuri yetu ya Kenya. Nilibahatika kuwa mmoja wa wanakamati ambao walikuwa wanamhoji Eng. Koome. Tuliona ana tajiriba kubwa kutokana na utendakazi wake humu nchini. Bila shaka ni mtu aliye na uzoefu wa kufanya kazi. Atakapopewa nafasi ya kutumikia wananchi wa Jamhuri ya Kenya, naamini ya kwamba atafanya kazi nzuri na kutuhakikishia usalama wetu. Natoka katika Kaunti ya Lamu ambapo kwa muda mrefu tumekuwa na shida ya usalama. Nina uhakika kwamba Eng. Koome anajua jinsi atasaidia watu wangu wa Kaunti ya Lamu na kuona kwamba hali ya usalama inaimarika. Bw. Naibu Spika, watu hutoka Kenya na kwenda nchi za Waarabu kutafuta kazi ili wajipatie riziki. Tumekuwa tukisikia visa tofauti tofauti katika nchi za Waarabu. Baadhi ya watu wetu wanarudishwa wakiwa wamefariki kwa sababu ya maisha magumu katika nchi hizo. Nina uhakika kwamba Eng. Koome atahakikisha kuwa watu wetu wanaokwenda nchi za ugenini kutafuta kazi watakuwa sawa. Watu wetu wanapokwenda huko ugenini, pasipoti zao huchukuliwa na waajiri wao. Kuna tatizo la ulevi wa kupita kiasi hapa nchini ambao umewaharibu vijana wetu. Hilo ni jambo ambalo Eng. Koome anafaa kuzingatia sana ili kuhakikisha kwamba ulevi wa kupindukia umepunguzwa kwa sababu unazorotesha uchumi wa Jamhuri ya Kenya. Nina hakika kuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa ya usalama hapa nchini, Seneti ikiidhinisha Eng. Koome kuwa inspekta mkuu wa polisi. Nina imani ataleta"
}