GET /api/v0.1/hansard/entries/1193058/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193058,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193058/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa hapa ili tuijadili. Eng. Koome ni afisa ambaye amebobea katika mambo ya ulinzi hapa nchini. Siku za nyuma, alichangia sana kuweka nidhamu upande wa trafiki hapa Nairobi. Kuna jambo moja muhimu ningependa kulizungumzia na ninajua Maseneta wenzangu wataniunga mkono. Kuna polisi ambao wako na tabia ya kufanya eviction hapa nchini siku ya Ijumaa au Jumamosi. Wengi hufanya kazi hiyo usiku. Tunaomba Eng. Koome ahakikishe kwamba jambo kama hili halitatokea tena katika hii nchi yetu. Bw. Naibu Spika, siku za nyuma kama mwaka mmoja na nusu uliopita, kule Kaunti ya Kwale, sehemu inaitwa Diani, ardhi mmoja ilivamiwa na wananchi waliondolewa pale usiku wa manane wakati wa janga la korona. Hao watu hawakuwa na namna yoyote na hawangeweza kutembea usiku au kujisaidia kwa sababu kulikuwa na amri ya kutokutoka nje . Bw. Naibu Spika na waheshimiwa wenzangu, kweli kutakuwa na haki kama mtu yuko kwa ardhi na anatolewa usiku wa manane hapa nchini? Hili liwe jambo la kwanza ambalo Eng. Koome atalishughulikia akichaguliwa kuwa IG. Ahakikishe ya kwamba hakuna mtu anayetolewa katika ardhi yake usiku. Hili jambo ilitokea katika Kaunti yangu ya Kwale. Nyumba karibu 800 au 900 zilivunjwa wakati wa janga la korona, askari wakiangalia. Namtakia kila heri. Akipata hii kazi, ahakikishe jambo la watu kuvunjiwa nyumba na kutolewa katika ardhi zao usiku likome. Naunga mkono hoja hii."
}