GET /api/v0.1/hansard/entries/1193081/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193081,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193081/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, asante kwa kunipa fursa hii, kuunga mkona Hoja ya kumuidhinisha IG Koome kama Inspekta Mkuu wa Police. Sina ufahamu wa kutosha kumhusu bwana huyu. Hata hivyo, niko na imani kulingana na mtaala wake na ukaguzi uliofanyika, ataweza kuifanya hii kazi na kubeba hili jukumu kikamilifu. Katika kitengo cha polisi, kuna changamoto nyingi sana zikiwemo hongo na ufisadi. Ni tumaini yangu kwamba bwana huyu ataweza kupambana na ufisadi na hongo ambao ni donda sugu katika nchi yetu ya Kenya. Imekuwa ni aibu. Wakati wageni wanapofika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta au popote barabarani, wanaitishwa hongo kiholela na polisi. Bw. Naibu Spika, kuna misako isiyoeleweka ya kiholela inayoendelea hapa nchini. Utakuta polisi wanapokuwa hawana hela mifukoni au wakati mwezi upo ‘kona,’ wanaanza misako ya kiholela, wakisumbua wananchi, na kuokota pesa kwa njia isiyo halali. Kwa hivyo, hilo ni jambo ambalo tunaomba liangaziwe na Inspekta Mkuu wa Polisi. Kunao polisi wanaodhalilisha wananchi bila sababu. Wanawabeba wananchi na kuwafungia bila sababu za kueleweka. Wanachukua fursa hiyo kwa sababu wananchi wengi hawaelewi sheria na haki zao kiukamiilifu. Kwa hivyo, hayo ni mambo yanayoendelea sana hapa nchini. Pia polisi wanatumika vibaya. Nikitaka mtu yeyote ashikwe sasa hivi, ninaweza kuwapa pesa polisi na watafanya hivyo na pengine mtu huyo hana hatia na wamfungie ndani bila kufuata sheria. Kwa hivyo, kuna mambo mengi ambayo siyo ya kisheria yanayofanywa kimabavu na kiholela na polisi ambayo inafaa iangaliwe. Niko na imani kwamba inspekta anayekuja ataweza kukabaliana na hiyo changamoto ili sekta ya polisi iweze kunyooka. Ataifanya iwe ni sekta ambayo inaeleweka na kutoa huduma na utumishi kwa wote."
}