GET /api/v0.1/hansard/entries/1193100/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193100,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193100/?format=api",
"text_counter": 226,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Kwa wale ambao tumeishi nchini Kenya kwa miaka mingi, tunajua kuwa ukianzisha biashara yoyote, polisi ndio hupata faidi kubwa. Kama ni biashara ya daladala, utakuta polisi wako. Nashukuru kwa kuwa alisema kuwa akiwa IG, sare za askari hazitakuwa na mifuko. Hiyo itasaidia kuondoa uchukuaji ama upokeaji wa hongo kwa polisi barabarani. Utoaji hongo ni jambo linalochangia kupunguza faida ya biashara ya matatu. Wale walio na biashara ya vilabu pia huangaishwa sana na maaskari. Janga lolote likitokea, wao pia hujaribu kuona jinsi ya kunufaika. Nakumbuka sheria za kuzingatiwa wakati wa korona zilipowekwa, kule kwetu kuna maaskari waliokuwa wanafukuza watu kwa sababu ya kutovaa barakoa. Nashukuru Mungu kwa kuwa kuna gari aina ya Land Rover lililopata ajali na maaskari waliumia."
}