GET /api/v0.1/hansard/entries/1193102/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193102,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193102/?format=api",
"text_counter": 228,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Ni vyema kufurahi mambo mengine yakitendeka kwa sababu ajali kama hizo ni za kujitafutia. Je, mtu anafaa kuvaa barakoa akiwa shambani? Kwa sababu ya mazingira ya kufanya kazi na mtazamo wao kuwa lazima wapate kitu kidogo, siku hiyo walipata hasara. Mhandisi Koome anafaa kuangazia mazingira ya kazi ya maafisa wa polisi kwa sababu kazi wanayofanya ya kutulinda siyo rahisi. Kulingana na sheria, hawaruhusiwi kujiunga na vyama vya wafanyakazi au trade unions. Itabidi aangalie masuala ya utendakazi wa maafisa wa polisi kwa sababu wanatusaidia katika usalama na kukabiliana na vitendo vinavyochangia kuwe na utovu wa usalama. Nafikiri kuwa kuna motisha kidogo wa kufanya kazi kule kwetu na ndio maana kuna wizi mwingi. Ukienda kuripoti kisa cha wizi, hakuna wanachofanya kwa haraka. Sababu wanazotoa ni kuwa hawana petroli au gari ni moja na limetoka. Mambo kama hayo ya kukosa vifaa vya kufanyia kazi vinaleta utepetevu wa utenda kazi wa hawa maafisa wetu. Ningependa kuachia hapo na kuunga mkono ripoti hii ambayo inapendekeza kuteuliwa kwa Mhandisi Japheth Koome kuwa Inspekta Generali wa Polisi."
}