GET /api/v0.1/hansard/entries/1193108/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193108,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193108/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "Ahsante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia na kucongratulate IG kwa uteuzi wake. Nataka kumpongeza na maafisa wote wa polisi kwa ajili ya kazi nzito ambayo wanafanyia taifa hili. Polisi wanafanya kazi nzito sana. Wakati ambapo mvua inanyesha, wao huwa inje wakichunga wananchi. Wao huwa nje usiku pia wakichunga wananchi. Mara nyingi, huwa tunaona tu yale mambo madogo ambayo wanatenda lakini hatuoni mambo makubwa ambayo wanatendea taifa kwa sababu polisi wamejitolea kufanya kazi. Mara nyingi wanahatarisha maisha yao. Wanaposikia kuwa hatari imetokea mahali fulani, huwa wanakimbia pale kuangalia kile ambacho kimetokea. Tumepoteza askari wengi kupitia mambo kama hayo. Wengi wao huwa wanauawa wakienda sehemu za Turkana na kule ambapo kunakuwa na cattle “hustlings” ---"
}