GET /api/v0.1/hansard/entries/1193119/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193119,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193119/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13733,
        "legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
        "slug": "agnes-kavindu-muthama"
    },
    "content": "Ahsante, Bw. Naibu wa Spika. Ninamshukuru mwenzangu lakini hata yeye amekosea akimaliza. Polisi wanafanya kazi mzito sana. Kwa hivyo, ninamwombea huyu IG mpya ambaye ameteuliwa na Raisi wetu, (Dr.) Wiliam Samoei Ruto, ili aweze kuwa na uvumilivu kwa sababu hii kazi sio rahisi. Huwa wananyoshewa kidole cha lawama mara nyingi ilhali hao pia ni binadamu kama sisi. Ningeomba pia aangalie maslahi ya polisi wenzake haswa jinsi wanavyoishi kule mashinani. Nyumba ambazo afisa wa polisi wanaishi ni duni kabisa na hata watu wanaosemekana kuwa wanafanya kazi hawastahili kuishi humo. Ninaomba pia Serikali yetu iweze kuangalia maslahi ya polisi. Itakuwa vyema kama Serikali itawajengea nyumba nzuri na kuwapa mahali pazuri pa kutendea kazi ili hao pia waweze kufanya kazi yao wakifurahi kama watu wengine ambao wameajiriwa. Mimi ninamcongratulate IG. Tunamwombea ili aweze kufanya kazi kwa bidii na kutimiza wajibu wake kwa taifa letu la Kenya. Asante."
}