GET /api/v0.1/hansard/entries/1193134/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193134,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193134/?format=api",
"text_counter": 260,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw . Spika, kwa kunipa nafasi hii pia nami nitoe kongole yangu kwa ndugu yetu, Eng . Koome. Natoa kongole kwa Eng. Koome ambaye ni Inspekta Jenerali wa Polisi mteuliwa. Katika rekodi zake ni kwamba yeye ni kati ya wale watu waliweza kwenda chuo kikuu na kupita na shahada ya uhandisi. Hatimaye, aliweza kukubaliwa kuingia jeshi kwa sababu ilikuwa ndio mfumo wa kwanza. Hii inamaanisha kwamba nia yake yote katika usomaji hata akifanya Engineering, alikuwa anaweza kuwacha mambo ya engineering ama akajiendeleza kidogo akiwa huko. Kuna mambo mengi pia yanafanyika ndani ya polisi kama mambo ya ujenzi kidogo lakini hususan hiyo si kazi ya polisi. Yeye alipokuwa katika hiyo shughuli ya kusoma ilikuwa nia yake kuwa polisi. Amekuwa polisi kwa muda huo wote hadi sasa ambapo ameteuliwa Inspekta Jenerali wa Polisi katika Kenya. Hilo ni jambo la kumpatia kongole sana."
}