GET /api/v0.1/hansard/entries/1193138/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193138,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193138/?format=api",
    "text_counter": 264,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "kwenye meza yake. Tumeonelea kwamba watoto wetu, hususan watoto wengi sana wa Kiislamu wamepoteza maisha yao katika sehemu za Pwani na kwingineko katika nchi ya Kenya. Watoto wetu waliweza kuwekwa katika vitengo vya wale wahalifu ambao wanafanya matendo machafu na wakashikwa bila kuwa na ushahidi wowote. Hii ndio sababu wakishikwa, ikiwa polisi hawana ushahidi wowote, walikuwa wanawekwa katika hayo maboksi ambayo walikuwa wakisema yako ndani ya vituo vya polisi, halafu mtu anapoteza maisha yake pale. Mara nyingi tukiwa hapa, tumekuwa tukiuliza maswali ya wale watoto wetu wanaopotea katika mikono ya polisi. Wakati mwingine tunaona magari yanapita, video inachukuliwa na mtu anatolewa katika gari hii na anasukumwa katika lingine. Wale wanaofanya videndo hivyo wote wanajulikana ni mapolisi lakini hakuna hata polisi mmoja atakayeulizwa ama kupelekwa mahakamani na kuambiwa kwamba, “wewe ndio ulikuwa pale na ulipatikana katika hii video, huyu mtu alikwenda wapi?” Hakuna mtu anayeulizwa na jamii inaachwa ikilia na kupata taabu kwa sababu mzee wao alihukuliwa na kuchukuliwa na polisi na kupoteza maisha yake. Vilevile polisi wana tabia mbaya sana kufikia hivi sasa. Wao wanashika watu ovyo ovyo hata kule pande zangu kule Mtwapa na mjini Kilifi. Inajulikana kwamba sisi watu wa Mtwapa tuko na “ 24 hours’ economy” ambayo hiyo ni sawa kabisa. Tunatengeneza hii nchi tukiinua uchumi."
}