GET /api/v0.1/hansard/entries/1193142/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193142,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193142/?format=api",
"text_counter": 268,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Watu kushikwa kiholela usiku katika maeneo yao ya burudani ni jambo ambalo tunaliona sana. Mtu kitoa kitambulisho vilevile anaambiwa lazima atoe “kitu kidogo”. Hiyo mambo ya kitu kidogo tunataka ikome sasa. Yeye mwenye anaitwa Eng. Koome na hiyo sisi tanataka ikome. Tuna imani ya kwamba pahali alipo nina hakika anaweza kuangalia na akajua kwamba Seneti inamwambia akomeshe hiyo taabia mbaya ya hao watu wake walio huko chini. Wale polisi wadogo wadogo wakome kuchukua hongo ama kusumbua watu katika maeneo yao ya burudani. Jambo la kusisikitisha sana ni kuwa kuna ulevi mwingi sana ambao unafanywa katika vitengo vya chini vya askari hata vitengo vya juu. Wakati mwingine polisi wa chini sergeant anaweza kuchukua bunduki akapiga bosi wake kwa sababu bosi amemwambia aende katika eneo fulani akaangalie mambo ya usalama. Yeye anakasirika, anachukua hiyo bunduki aliyonayo na kumpiga risasi huyo mkubwa wake."
}