GET /api/v0.1/hansard/entries/1193184/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193184,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193184/?format=api",
    "text_counter": 310,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Ahsante, Bw. Spika. Nasimama kuunga mkono Mswada huu ambao umeletwa na Kiongozi wa Wengi. Ni wazi dhahiri shahiri kwamba mimi ni mmoja wa wale wameteuliwa katika Tume ile. Kwanza kabisa, nataka kupongeza wale wengine walioteuliwa; Mhe. Mohamed Ali, Mhe. Faith Gitau, Mhe. Patrick Makau, Mhe. Joyce Korir na wale wengine wote. Hawa ni watu ambao wamemakinika kwa kazi yao. Mimi na wale wengine watakoingia kwa Tume hii tutaenda kuwakilisha Wabunge wala sio sisi binafsi. Bw. Spika, imekua ya kwamba mtu akichaguliwa katika Tume ile, yeye huenda kwa mapendekezo yake mwenyewe na kujipendelea. Tutafanya kazi na Wabunge wale wengine kwa sababu kunasemekana ya kwamba ukitaka kwenda mbali, utembee na wengine. Ukitaka kwenda haraka, enda peke yako lakini hata hivo, utasulubiwa peke yako. Nataka kuhakikishia Bunge hili ya kwamba inajulikana wazi Tume la Salaries"
}