GET /api/v0.1/hansard/entries/1193191/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193191,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193191/?format=api",
"text_counter": 317,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika, ni vizuri hawa ndugu zetu wa SRC wajue ya kwamba hata sisi tuna haki kisheria na tutafuata sheria mpaka tuangaliwe na wao pia wafanye kazi yao. Ukiangalia, hao wenyewe wamejiongezea mishahara maradufu. Sisemi sisi tunaenda kujiongezea mishahara lakini mtu alipwe kulingana na kazi aliofanya. Mbunge anafanya kazi usiku na mchana. Simu yake inapigwa asubuhi na usiku pia. Naonea huruma Maseneta wachanga walio hapa. Mhe. Madzayo, sijui kama watapata fursa ya kupata watoto kwa sababu simu zinapigwa usiku. Sijui kazi zingine na majukumu mengine yatafanywa vipi. Inakua ni vigumu kidogo."
}