GET /api/v0.1/hansard/entries/1193229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193229,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193229/?format=api",
    "text_counter": 355,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Kwanza, nashukuru kwamba waliochaguliwa kuhudumu katika Tume hii ni watu ambao tunawajua na tumefanya nao kazi. Uteuzi wa Mhe. Mishi Mboko, Mhe. Mohammed Ali - “Simba wa Nyali” - na Mhe. Joyce Korir, ni ishara kwamba, kwa mara ya kwanza, sisi viongozi wa Pwani tumedhihirisha kwamba tunaweza kuketi katika uongozi wa juu wa Bunge la Kitaifa. Sen. Joyce Korir ni Seneta Mteule kama mimi. Kwa hivyo, najihisi, mimi kama Seneta Mteule, niko sawia na Seneta waliopigiwa kura debeni. Ninawashukuru wenzangu kwa kumleta Sen. Omogeni katika Tume hii. Ni wakili aliyebobea na Seneta mchapakazi. Ilikuwa ni jambo mbaya, kumwona Sen. Omogeni akizama kupitia siasa potovu ya utapeli, chuki na wivu."
}