GET /api/v0.1/hansard/entries/1193233/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193233,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193233/?format=api",
    "text_counter": 359,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii, ili niweze kutoa shukrani zangu kwa Maseneta waliochaguliwa kuhudumu katika PSC. Bw. Spika, siku ya leo, tumeweza kutatua utata ambao ulikuwa unatukera sana, upande wetu. Hatukujua tufanye nini, lakini hivi leo tumemaliza shida iliyokuwa hapa. Sisi Maseneta tuna shida mingi sana. Ni lazima tupate mtu anayeweza kupigania haki zetu kule mbele. Kama ilivyozungumzwa na Sen. Cheruiyot, Maseneta wako na majukumu makubwa sana katika hali yetu ya kifedha na matatizo mengi. Ni lazima tupate Makamishna ambao watatutetea, ili tupate haki zetu. Maseneta wenzangu, Sen. Omogeni amebobea kisheria. Yeye in Senior Counsel. Niko na imani, akiingia kule, tutaongezewa masrufu yetu ya mileage, nyumba na kila kitu. Sen. Omogeni, ukifika kule, kaa ukijua tunangoja kuona mambo yakiwa mazuri. Sen. Cheruiyot alipokuwa pale, alipigania sana pesa za nyumba za wafanyikazi wa PSC. Niko na hakika pia wewe utakapoingia huko, utahakikisha mambo yetu imekuwa mazuri kabisa."
}