GET /api/v0.1/hansard/entries/1193433/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193433,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193433/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Leo nataka kusema kwamba NG-CDF ama Hazina ya Maendeleo Kwenya Maeneo Bunge imeniwezesha kujenga makao ya serikali ya Taifa kule Jomvu – yani sub-countyheadquarters, ambayo haikuweko zamani. Vile vile, NG-CDF imetuwezesha kujenga shule kama nyingi, kama vile Shule ya Msingi ya Maganda, sehemu ambayo haikuwahi kuwa na shule wakati wa nyuma. Watoto wetu walikuwa wakitoka Miritini na kuenda mpaka Kwale County, mahali panapoitwa Mwamdudu. Kufikia leo, nimejenga shule mahali pale, inayoitwa Maganda. Vile vile, nimejenga shule mahali panapoitwa Kibarani, ambapo palijulikana hatari na hapakuweza kufanywa maendeleo yo yote. Kuna mahali ambapo sisi tunapakana na Rabai, ambako kulikuwa hakuna shule ya upili. Nimejenga shule ya upili inayoitwa Miroroni. Mimi niko na wodi tatu. Pesa za Maeneo Bunge zimeniwezesha kuweka polisi katika kila eneo kwenye wodi zangu. Vilevile, namshukuru Mungu kwa sababu pesa hizi zilituwezesha kujenga Ofisi za Assistant County Commissioners na machifu katika kila kata. Wabunge wengi wameongea kuhusu watoto kusomeshwa. Leo nasema mtoto wa kike na wa kiume wanastahili kusomeshwa. Ninafuraha kubwa sana kwa ajili wewe ambaye ni Naibu wa Spika wetu ndiye uliyemuapisha Rais Uhuru Kenyattta kule Kasarani ukiwa Registrar wa Mahakama Kuu. Nina imani kuwa hungeweza kuwa Registrar wakati ule kama siyo elimu yako ambayo imekuwezesha kufikisha pale. Tunakumbuka wakati ulipokuwa kamishna katika Tume ya Uchaguzi. Tuna imani kuwa ni elimu yako ndiyo iliyokufikisha pale. Wewe uko hapa kama Naibu wa Spika ambaye anaendeleza vikao vya Bunge. Naamini kuwa ni elimu ambayo imeweza kukufikisha hapa. Nina imani kwamba Rais wa kwanza wa kike nchini Kenya atakuwa wewe kwa ajili ya elimu uliyonayo."
}