GET /api/v0.1/hansard/entries/1193434/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193434,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193434/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Pesa za Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge zimefanya mambo mengi. Mwanafunzi bora zaidi katika mutihani wa kitaifa wa Darasa la Nane katika eneo la Pwani mwaka jana alitoka shule ya Amani Primary School. Tulimpatia scholarship tukitumia edha za NG-CDF ndiyo tukaweza kumpeleka kule Kisumu mahali alipopata shule. Ilikuwa furaha manaake mama yake hakujua jinsi angeweza kuendeleza elimu ya msichana yule anayeitwa Lisa Adhiambo. Hakujua angepata wapi pesa ili ampeleke shuleni. Lakini kupitia kwa ofisi ya mjumbe, tulimlipia karo ya mwaka mzima. Pia, ili kuweza kumtia motisha msichana yule, tulimkatia tikiti ya ndege kutoka Mombasa hadi Kisumu. Kwa hivyo, nina imani kwamba hii ni njia moja ambayo imetumewezesha kubadilisha maisha ya watu wengi. Wazo hili la kuweka sheria ya hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge katika Katiba litawakomesha wale watu ambao shughuli yao ni kupinga kila linaloendelea katika Bunge hili. Kuna watu wengi waliotupeleka kortini mara nyingi, kama alivyosema Mbunge wa Tigania Kaskazini. Hata hivyo, tuliweza kupambana na watu hao kortini. Mhe. Mule na Mhe. Gichimu wanaweka historia. Tutakapostaafu kutoka ulingo wa siasa, watakaochukua uongozi katika maeneo Bunge hawatasumbuliwa tena kwa sababu hazina ya NG-CDF itakuwa inalindwa na Katiba yan chi. Vile vile, majina ya Wabunge hawa wawili yataingia kwenye kumbukumbu za historia ya Kenya kwa kupingania kuendele kuwepo kwa hazina ya NG-CDF. Nasi pia tutaingia kwenya historia kuwa tuliweza kuunga mkono mambo kama haya."
}