GET /api/v0.1/hansard/entries/1193548/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193548,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193548/?format=api",
    "text_counter": 273,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, nilikuwa natangulia kusema kwamba nashangazwa sana na watu ambao wanapinga maswala ya NG-CDF. Kama kuna Mkenya yeyote anayepinga maswala ya NG-CDF, anapinga kwa misingi gani? Na ni suluhisho lipi wako nalo kuhakikisha wanafunzi milioni moja kila mwaka wanasaidika katika shule zao tofauti tofauti. Nashangazwa na hao watu. Kivipi hawaoni maendeleo ya madarasa zaidi ya elfu ishirini na moja ambayo yamejengwa kupitia NG-CDF? Hawa watu wananishangaza. Ombi langu kwa Wabunge wenzangu ni kwamba hizo ni kelele za chura, zisituzuie kunywa maji. Ni lazima tufanyie wananchi wetu kazi na ni lazima tupitishe maswala ya NG-CDF na NGAAF na tuyaweke kwenye Katiba ili kuhakikisha kwamba matatizo madogo madogo kama haya hayatukumbi huko mbele katika maisha yetu. Jambo la kwanza ningependa kusisitiza ni majengo bora. Kama mnavyoona, Kenya yetu imebadilika. Zile enzi za watoto na wanafunzi kuketi chini huku wanasomeshwa chini ya mti zimepitwa na wakati. Hayo yote yamesaidika na kuondolewa kupitia huu mfuko wa NG- CDF ambao Wabunge wako nao. Mimi naunga huu mjadala mkono kwa sababu najua kuna mambo makubwa yametendeka eneo bunge langu la Malindi. Sio shule pekee yake. Kuna masoko. Akina mama wanatoka katika nyumba zao huku wamebeba mizigo yao na biashara zao wakichuuza chini ya kiangazi. Leo hii wako ndani ya nyumba kwa sababu ya NG-CDF. Serikali iliyoko leo inasema ni Hustler Nation. Na mahustler ni kama hao mama mboga ambao wako hapa nchini. Tukiondoa NG-CDF, majengo ya hao akina mama yatajengwa na akina nani? Kuna jambo la pili ningependa kuliweka wazi - ya kwamba sisi Wakenya ni wazalendo. Na ni wakati sisi kama wakenya na viongozi tufanye jitihada na mambo ambayo yatafanya tupende pia wale Wakenya wa chini kabisa. Wakenya kwa dakika hii wanahitaji huduma bora na za haraka. Ni NG-CDF imeweza. Tumeona kwa mifano mingi ambayo wenzangu wameshatangulia kuzungumzia. Ya kwamba kupitia NG-CDF, huduma bora na huduma za haraka zinaweza kuwafikia wananchi. Mfano ni huu: Katika matatizo yeyote katika eneo bunge la mbunge yeyote, ni Mbunge aliye mtu wa kwanza kutatua matatizo yaliyo hapo. Leo hii tukisema tunaondoa NG-CDF na kuleta maendeleo hayo yote kwa Serikali kuu, unafikiria ile shule inayotaka kuporomoka itakuwa imemalizika kitambo zile pesa zifike ndani ya hiyo miaka yake mitano? Kupitia NG-CDF, tumekuwa na huduma bora na za haraka pasipo kusahau zile kazi ambazo watu wameweza kuajiriwa kupitia NG-CDF. Saa hizi tuko na matatizo katika Kenya hii. Kuna watu wengi ambao hawana ajira. Masuala ya ajira yamekuwa ni donda sugu kabisa. Mbali na ile ofisi ya NG-CDF iliyo hapa Nairobi, wameajiri watu na tukisema tunaondoa NG- CDF, tunataka ndugu zetu waishi vipi? Mbali na hayo, katika kila eneo Bunge, kuna wafanyikazi walioandikwa kupitia NG-CDF. Hazina ya NG-CDF ikiondolewa, hao ndugu zetu tunawaelekeza vipi katika maisha yao? Ndiyo maana tunasema kwa niaba ya watu wa Malindi kwamba NG-CDF, mjadala ulio hapa leo, uweze kupitishwa haraka sana."
}