GET /api/v0.1/hansard/entries/1193549/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193549,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193549/?format=api",
    "text_counter": 274,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, kuna matatizo ya elimu; hasa ukosefu wa karo miongoni mwa watoto wetu kule mashuleni. Kama nilivyotangulia kuzungumza, wanafunzi zaidi ya milioni moja wanaweza kusaidika kwa njia tofauti tofauti kupitia bursary. Wanafunzi kama hao tunawaelekeza wapi? Tunawapatia mbinu gani mbadala kama sio kwa kutumia pesa za NG- CDF? Ninavyozungumza, kuna wanafunzi zaidi ya elfu tano ambao wanaenda kufanya mtihani wao wa kitaifa. Na siyo wote walio na uwezo wa kujisaidia. Zaidi ya asilimia sabini ya wanafunzi wanaokwenda kufanya mtihani katika eneo Bunge la Malindi, ni watu ambao hali zao ni duni. Tusipowashika mkono, tutakuwa tumeyapoteza maisha ya watoto wetu. Ndiyo maana tunasema tunaunga mkono Mswada ulio hapa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}