GET /api/v0.1/hansard/entries/1193550/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193550,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193550/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa kumalizia, NG-CDF imeleta mazingira bora kwa watu wanaofanya kazi mashuleni na vituo vya polisi tofauti tofauti katika Kenya. Nakumbuka mradi wangu wa mwisho ambao nimefanya Malindi, hata kabla sijapata kiti cha Ubunge, ni kujenga vyoo katika shule ya upili ya Maziwani ambayo ina wanafunzi zaidi ya mia sita. Kuna walimu wa kike na wa kiume. Hao watu walikua wanaenda haja zao kubwa na ndogo msituni. Ndiyo maana tunasema tunataka jambo hili tuliweke katika Katiba ili maendeleo yazidi kufikia wananchi wetu katika maeneo bunge tofauti tofauti. Kwa niaba ya watu wa Malindi, naunga Mswada huu mkono asilimia mia moja. Kwa hayo machache, ahsanteni."
}