GET /api/v0.1/hansard/entries/1193553/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193553,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193553/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, nachukua fursa hii kwanza kukushukuru wewe na kukupongeza kwa kunipa fursa mimi nitie sauti yangu katika swala hili. Naunga mkono marekebisho ya Katiba kuihalalisha NG-CDF katika Katiba iwe haitasumbuka na kusitokee mtu kwenda kuishtaki ama kuilalamikia. Iwe iko ndani ya Katiba na iwe ni sheria kwamba hizi fedha ziwe zinakuja bila kuwa na kikomo wala hofu. Mengi yamezungumzwa lakini mimi pia nitatia sauti yangu hapo. Hakika, NG-CDF ni hazina ambayo imesaidia wananchi. Kenya ni taifa ambalo wengi wa wananchi hawana ajira na wengi ni maskini. Wenye uwezo ni wachache. Wengi wanashindwa hata kunywa chai. Wengine wana watoto wawili au watatu walio shule. Inakuwa ni vigumu kwa yule mzazi kupata karo ya kuwasomesha watoto wale. Ndiyo maana nasikia wengine wanaambiwa wakae nje wachunge mbuzi, na mmoja anaenda kusoma kwa niaba ya wale wengine. Hazina hii ya NG-CDF imemsaidia hata maskini kuwa na matumaini ya kupata elimu ya msingi na kuenda shule ya sekondari na hata vyuo vikuu. Maskini ana imani kwamba kuna mgao fulani ambao utamsaidia kusukuma elimu yake iwe sawa na wale walio na uwezo. Wale ambao wanaenda kuishtaki NG-CDF kuwa ni hazina isiyo halali na wanataka itolewe ni watu wa kushangaza sana. Sijui kama wanaishi katika taifa hili ama ng’ambo, ama wana uwezo mkubwa na hawajali maskini. Watu wengi wameamka asubuhi, hata chai hawana. Badala ya kuishtaki iondolewe, wangeenda kuitilia nguvu na kusema kuwa NG-CDF iongezwe iwe na uwezo hata wa kuwanunulia watoto wetu chakula katika shule ili wanywe chai ama uji saa nne na saa sita wapewe chakula. Wangeenda kusema hivyo badala ya kusema itolewe. Maandishi “NG-CDF” yako katika majengo yote yanayopatikana katika maeneo Bunge yetu, kuonyesha kuwa kama NG-CDF haingekuwepo, majengo hayo hayangekuwapo. Pia, ikiwa NG-CDF itatolewa, Wajumbe hawa watategemea kwenda kwenye milango ya Executive kila Jumamosi kuomba kabla ya kwenda mashinani. Tukianza kuomba, tutafanya oversight namna gani? Ikiwa Mjumbe ako na NG-CDF, hana sababu ya kwenda kuomba kutoka kwa"
}