GET /api/v0.1/hansard/entries/1193556/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193556,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193556/?format=api",
    "text_counter": 281,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "CDF, mambo ya usafiri yangekuwa katika shule za kibinafsi pekee. Naomba kuwa NG-CDF ibakie ili isaidie. Ihalalishwe kwenye Katiba ili iendelee. Si vibaya hata hawa ndugu zetu Maseneta wakipewa fedha, bora zimfaidi mwananchi. Wakati mwingine unasikia Serikali ikisema kuwa uchumi umeimarika. Uchumi hauwezi kuimarika kama mwananchi hana kitu mfukoni mwake! Lazima uchumi uhusiane na mwananchi. Kwa hivyo, hata wale Maseneta wakitaka fedha za kuwasaidia wananchi, wapewe. Ikiwa zile fedha Wawakilishi wa Akina Mama watapewa zitasaidia, itakuwa vizuri zaidi. Ikiwa Wawakilishi wa Akina Mama, Wajumbe na Maseneta watasaidia, wananchi ndio watafaidika. Hili ni taifa letu sote. Kwa hivyo, ni lazima tushirikiane kuhakikisha kuwa mwananchi anaishi salama na ana mambo rahisi katika mazingira ya kitaifa. Najua kuna wengi wanaosubiri kuzungumza na, kwa hivyo, sitaki niende mbali zaidi. Natoa fursa kwa wengine pia wazungumze. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}