GET /api/v0.1/hansard/entries/1193587/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193587,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193587/?format=api",
    "text_counter": 312,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Embakasi South, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Julius Mawathe",
    "speaker": null,
    "content": "Ningetaka kuanza kwa kusema kwamba naunga mkono Hoja hii ya kusema NG-CDF iwekwe katika Katiba. Ndiposa wanaofikiria watashinda wakizungumza na kusumbua wananchi kwa kwenda kortini, jambo hilo liishe mara moja. Hiyo ni kwa sababu wakati mmoja waligusia aliyekuwa Waziri wa Fedha, Ukur Yatani, kwa kusema kuna ruling ambayo ilitolewa kuhusu NG-CDF. Nataka kukosoa kwa kusema kwamba NG-CDF haijawai kupelekwa kortini na mtu yeyote. Iliyopelekwa kortini ni sheria ya 2013 ambayo ilikuwa inaitwa Sheria ya CDF ya 2013. Hiyo iliisha na ikatengwa sheria mpya ya NG-CDF. Kwa hivyo, hakuna ruling yoyote ambayo imetolewa kuhusu NG-CDF ambayo ni muhimu sana kwa wengine wetu. Mimi ni mwakilishi wa eneo Bunge ambalo zaidi ya asilimia 80 ni watu wa mapato ya chini. Hazina ya NG-CDF imewasaidia sana. Kuipitia tumejenga shule tatu. Hapo mbeleni, licha ya Embakasi Kusini kuwa katika Nairobi Kaunti, ilikuwa na shule moja ya serikali ya sekondari peke yake inayoitwa Embakasi Girls. Hili ni jambo la aibu sana. Sisi tulikuwa tunaenda shule za majirani. Hatukuwa na shule zetu. Lakini kupitia NG-CDF, tumejenga shule kama vile Reuben Sekondari, Kware S ekondari, Kware Primary na nyinginezo. Pia tumejenga dorms zenye vitanda 450 katika Embakasi Girls. Watu huniita mtaani, ‘Mtu wa bursary’ ama ‘Watoto wasome’. Kama sio NG-CDF, hao watoto wangekuwa wanasoma na nini? Watoto wengi hawakuwa na nafasi ya kwenda shuleni. Lakini kupitia NG-CDF, wanaenda shuleni vizuri, kwa sababu wanapatiwa bursary za masomo. Wanaopinga hili jambo la NG-CDF ni mabwenyenye na matajiri. Wako na pesa za kupatia lawyers waende kortini. Hawajali mwananchi wa kawaida ambaye hana mapato. Atawasomesha watoto wake kwa kutumia nini? Mwaka jana, watoto zaidi 1,133 wali graduate kutoka universities . Walianza kusoma miaka minne iliyopita kupitia bursary. Tumefanya mengi kupitia NG-CDF na nina uhakika kwamba itaendelea kuwepo. Tunaomba iongezwe kutoka asilimia mbili nukta tano mpaka asilimia tano kama itawezekana, ama watakavyokubaliana kama alivyosema mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi. Isipungue asilimia nne lakini iwe katikati ya asilimia nne na tano. Tuko tayari kuzungumza na wao ndiyo tuweze kuendelea kupata NG-CDF. Pia tunapigia debe kuwepo kwa hazina ya Seneti ya oversigh t, na NGAAF ndiyo Women Representatives wetu wapate pesa za kuwahudumia wananchi wetu. Pia, tunapigia debe Uwezo Fund ndiyo vijana na akina mama waweze kupata senti za kuanzisha mabiashara. Kwa hayo mengi, naunga mkono hii Hoja ya kuweka NG-CDF katika Katiba. Ahsante sana."
}