GET /api/v0.1/hansard/entries/1193880/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193880,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193880/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Majority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Spika, kwanza, ningependa kuwapongeza wale waliochaguliwa kutuakilisha katika Bunge la Afrika ambalo makao yake yako kule Johannesburg, Afrika Kusini. Wa kwanza kwenye list hii ni Sen. (Prof.) Kamar ambaye alifanya kazi nzuri alipokuwa mhadhiri katika chuo kikuu Cha Moi. Ni mtu aliye na taaluma na tajiriba ya kufundisha na tuna imani ya kuwa atatuakilisha katika Bunge la Afrika. Wa pili ni Sen. Mungatana, MGH. Ninavyoelewa ni wakili mkubwa katika taifa letu la Kenya. Amekuwa katika Mbunge nafikiri kwa zaidi ya miaka 10. Huu ni muhula wake wa tatu. Sijui kama nimekosea lakini nina imani na rekodi zangu. Natumai atatia juhudi wakati anatuwakilisha katika Bunge la Afrika. Vile vile kuna Mhe. Rahab Mukami, Mhe. Joseph Kalasinga na Mhe. Esther Muthoni Passaris. Nina imani kwamba wote, haswa wenzetu hapa, watatuwakilisha vyema. Niliwakilisha taifa la Kenya katika Bunge hilo. Ni Bunge la hali ya juu sana. Nina imani kwamba wenzetu watakuwa wanatueleza yanayojiri katika Bara la Afrika. Bw. Spika, kwa hayo machache, ninaunga mkono uteuzi wao."
}