GET /api/v0.1/hansard/entries/1193885/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193885,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193885/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Methu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13581,
"legal_name": "Methu John Muhia",
"slug": "methu-john-muhia"
},
"content": "Kwanza, naunga mkono Hoja ambayo imeletwa na Seneta wa Kakamega, Sen. (Dr.) Khalwale. Nikiangalia kwa makini, waheshimiwa wote watano kutoka pande zote mbili wana tajiriba. Wa kwanza kwenye orodha ni Sen. (Prof.) Kamar ambaye alihudumu kama Mbunge, Seneta, Naibu wa Spika, Waziri wa Elimu ya Juu na Naibu wa Waziri wa Mazingira. Kwa hivyo ana tajiriba ya juu sana. Seneta wa Kaunti ya Tana River amekuwa Mhe. Mbunge kwa miaka mingi. Nimemkumbusha siku nyingi kwamba alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mhe. Mbunge, mimi nilikuwa katika darasa la nne. Kwa hivyo, ana tajiriba ya juu sana. Kulingana na mafunzo tuliyopata juma lililopita, wao wataenda kule kutuwakilisha sisi sote. Wataenda katika Bunge la Afrika kwa niaba yetu. Kwa hivyo, watakuwa wanatuarifu yanayojiri katika Bunge la Afrika. Bw. Spika, tulikuwa tumekutuma kwenda kufanya kazi ya kimataifa na ulituwakilisha vizuri. Sitaki kusema zaidi ya hapo kwa sababu naweza kuharibu. Asante."
}